IF YOU FAIL TO PLAN,YOU PLAN TO FAIL

Kituo cha elimu Soni falls kipo ktk milima ya usambara, kijiji cha Soni wilayani Lushoto Mkoani Tanga,Nchini Tanzania.ukifika Soni kisiwani kituo kipo jirani na kanisa la KKKT Usharika wa soni kwenye majengo yaliyokuwa yakitumika  kama hotel iliyokuwa ikifahamika kwa jina  Old soni falls hotel ni Km15 kutoka Mombo njia kuu ya Arusha, Moshi,

Majengo ya Soni falls ni kati ya vivutio vya kitalii vilivyopo usambara (Historical site ) Majengo ya soni falls yamejengwa mwaka 1935 na mmiliki wake wa kwanza aliitwa Von Lico alikuwa ni mjerumani ndipo baadae iliuzwa kwa mzalendo,na hapohapo ndipo kilipo kivutio cha maporomoko ya maji soni  ( Soni Waterfalls )

Kituo kimeanzishwa mwaka 2010 kwa  lengo la kutoa elimu kwa wakazi wa soni na wale walio nje ya soni pia kuiunga mkono serikali katika jitihada za kuielimisha jamii yetu ili kupambana na adui ujinga

Kituo kimesajiliwa na Baraza la Mitihani Tanzania ( NECTA ) kwa namba P .4632

Elimu itolewayo katika kituo hiki ni ya kiwango cha juu walimu ni wahitimu kutoka vyuo mbalimbali vya ualimu hapa nchini na nchi za jirani ( Diploma and degree holders in education )

HUDUMA ZETU NI KWA;

  • Wanafunzi wanaorudia mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita
  • Wafanyakazi wanaopenda kujiendeleza ( Walimu,manesi,madaktari,nk )
  • QT (Qualified Test) – elimu ya sekondari kwa miaka miwili tu. (form one mpaka   form four )
  • Tuition kipindi cha likizo june na December
  • Pre-Form one course hii ni kwa ajili ya wanafunzi walio maliza elimu ya msingi  wanaojindaa kujiunga na elimu ya sekondari, kwa miezi mitatu

BASIC  APPLICATION COURSE;

Introduction to Computer

    • Ms -Word
    • Ms –Powerpoint
    • Ms -Excel
    • Ms-Publisher

Muda wa kozi ni wiki nane ( miezi miwili )

HOSTEL NA CHAKULA

Kituo pia kinatoa huduma  ya hostel na chakula kwa wale watakaopenda kubaki kituoni (boarding ) Kwa Wasichana  na Wavulana.

Matokeo ya mitihani ya kila wiki yatakuwepo kwenye tuvuti yetu.

kupakua fomu yetu bofya hapa chini (to download our form click the botton below)

FOMU YA KUJIUNGA 2013

KARIBUNI SANA

One comment

Leave a comment